Deuteronomy 32:35-43

35 aNi juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.
Wakati utakapowadia, mguu wao utateleza;
siku yao ya maafa ni karibu,
na maangamizo yao yanawajia haraka.”

36 b Bwana atawahukumu watu wake,
na kuwahurumia watumishi wake
atakapoona nguvu zao zimekwisha
wala hakuna yeyote aliyebaki,
mtumwa au aliye huru.
37 cAtasema: “Sasa iko wapi miungu yao,
mwamba walioukimbilia,
38 dmiungu wale waliokula mafuta ya dhabihu zao
na kunywa mvinyo wa sadaka zao za vinywaji?
Wainuke basi, wawasaidie!
Wawapeni basi ulinzi!

39 e“Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye!
Hakuna mungu mwingine ila Mimi.
Mimi ninaua na Mimi ninafufua,
Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya,
wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu.
40 fNinainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema:
Hakika kama niishivyo milele,
41 gwakati ninapounoa upanga wangu unaometameta
na mkono wangu unapoushika ili kutoa hukumu,
nitalipiza kisasi juu ya adui zangu
na kuwalipiza wale wanaonichukia.
42 hNitailevya mishale yangu kwa damu,
wakati upanga wangu ukitafuna nyama:
damu ya waliochinjwa pamoja na mateka,
vichwa vya viongozi wa adui.”

43 iFurahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake,
kwa kuwa atailipiza damu ya watumishi wake,
atalipiza kisasi juu ya adui zake
na kufanya upatanisho
kwa ajili ya nchi na watu wake.
Copyright information for SwhNEN